THIS PAGE HAS BEEN MOVED
If you are not redirected to its new location in a few seconds, please click here
DON'T FORGET TO UPDATE YOUR BOOKMARKS!
MAFUNZO
KAMA UHAMASHISHAJI
imetafsiriwa na Wamalwa Philip
Kijitabu
cha Mafunzo
Mbinu
za kukuza usimamizi wa jamii hujumulisha mbinu za maendeleo ya jamii na mafunzo ya
usimamizi wa jamii
Maana
Yetu Maalum ya "Mafunzo:"
Neno
"mafunzo" mara nyingi hufukiriwa kuwa ni kutoa ujuzi kwa wanafunzi. Kutia
moyo mwanafunzi huonekana kama ni jambo la kando tu. Katika mafunzo ya usimamizi
wa jamii, jukumu lake ni zaidi ya ile ya kuondoa umaskini na kujenga uwezo wa jamii.
Pia imeundwa kuhamashisha kikundi hicho kuchukua hatua mwafaka na usimamizi kuongeza
uwezo na nguvu.
Vipengele
muhimu ya neno mafunzo katika maana hii maalum in pamoja na:
- Kufahamisha;
- Kutoa
habari;
- Kusambaza
Ujuzi;
- Kusisimua
au kutia moyo;
- kuhamashisha;
na
- Usimamizi.
Ni
vipengele viwili vya mwisho ndivyo vinafanya mafunzo haya yawe maalum; mafunzo KAMA
uhamashishaji, si tu mafunzo KUHUSU uhamashishaji.
Kufahamisha:
Mafunzo
hutumika kama njia ya kuongeza ufahamu wa jamii kuhusu maswala kama ya kijinsia,
usafi wa mazingira, mafundisho kwamba umaskini si kusudio la Mungu au Majaliwa mbali
ni kitu ambacho kinaweza kubadilishwa na watu ikiwa wako tayari kuchukua hatua zifaazo.
Kuhamashisha
katika mafunzo ya usimamizi wa jamii inajumulisha kuvifahamisha vikundi vilivyolengwa
kuwa sisi sio msaada wa kutegemewa mbali tunatoa mafunzo ambayo yatawasaidia hao
wajisaidie wenyewe.
Kutoa
Habari:
Ikiwa
kutoa ufahamu utapelekea watu kuelewa vyema shida zinazowakabili (kwa mfano kwamba
hakuna usawa wa kijinsia na ambayo inazuia maendeleo), mafunzo huongezea kwa matokeo
hayo ya ufahamu kwa kutoa habari kuwa kuna suluhisho kwa shida hizo, ikiwa tu vikundi
vya washirika waliofundishwa vitakua tayari kuchukua hatua.
Kusambaza
Ujuzi:
Maana
ya kawaida ya "mafunzo," kwa mara nyingi huangazia tu kipengele hiki cha
kusambaza ujuzi. Hii humaanisha kuwa mwalimu hugawa ujuzi kwa wanafunzi. Maana maalum
ya mafunzo haitengi kipengele hiki cha kusambaza ujuzi, mbali inaangazia kwa makini
zaidi vipengele vingine vya mafunzo.
Ijapokuwa
ujuzi kama wa useremala na uashi au ujenzi ni muhimu, ujuzi huo hauhitajiki kwa dharura
katika jamii. Kile ambacho kinahitajika zaidi ni ujuzi wa kuhamashisha, wa kupanga,
kutambua rasilimali, kutambua matakwa na vipao mbele vya jamii, kuunda miradi, kuandika
mapendekezo na kuripoti (uazi). Kusambaza ujuzi huu wa usimamizi ni moja ya malengo
makuu ya mafunzo ya usimamizi wa jamii.
Kusisimua:
Kutia
watu moyo ili wajichukulie hatua wenyewe na wala sio tu kutumaini na kugonjea msaada
kutoka nje, hufanywa kwa kuvifahamisha vikundi vinavyofundishwa kuwa vina haki (au
hata jukumu) na uwezo wa kubadilisha vitu viwe vizuri.
Wanafahamishwa
kuwa wana mali yao na vipawa vyao, sio kulaumiwa, na wanapongezwa kwa mafanikio yao.
Huku kutia moyo hafanya watu kuwa tayari kuchukua hatua kwa niaba yao wenyewe na
hata kwa niaba ya jamii zao.
Ikiwa
kikundi au jamii imetiwa moyo zaidi, basi ni imara zaidi. (Tazama Vipengele
vya Kukuza Jamii).
Na,
hasa:
Uhamashishaji
na Usimamizi:
Kipengele
muhimu cha kufanya jamii iwe na uwezo zaidi ni kwa jamii hiyo kufanya vitendo. Kuunda
tu vikundi (na vyeo vya Mwenyekiti, Makamu, Mweka Hazina na Katibu kwa mfano) si
kitendo cha kutosha, hiyo ni njia ya kuandaa jamii kufanya jambo. Kuhamashisha kunamaanisha
kufanya jambo litendeke na matokeo kuonekana. Kwa hivo kujiandaa ili kuwezesha jambo
fulani kufanyika ni jambo muhimu katika mafunzo ya usimamizi.
Hii
ni mbinu ambayo inaleta pamoja mbinu kutoka nyanja mbali mbali, (1) usimamizi wa
vyama vya kutetea wafanyikazi na (2) mafunzo ya usimamizi wa maafisa wa ngazi za
juu wa makampuni kubwa kubwa. Yote mawili hayalengi tu kusambaza ujuzi kwa mtu binafsi
mbali katika kuunda vikundi vyenye uwezo na mafanikio makubwa. (Ili kujua tofauti
kati ya kujiandaa kwa ajili ya kutoa maamuzi na kujiandaa kwa ajili ya kufanya kitendo,
tizama sehemu ya mafunzo ya
Usimamizi).
Washiriki
wa mafunzo haya sio tu wanafunzi ambao wanapata ujuzi na habari. Ni washiriki ambao
tayari ni sehemu ya shirika, au wanatarajiwa kuwa sehemu ya shirika kwa sababu ya
mafunzo haya. Mafunzo hutumia mitindo kama ya "kuchangia mawazo"
(Tazama: Njia
za Kuchangia Mawazo)
ili kupata kutoka kwa washiriki hao nia na malengo ya kikundi, na njia bora zaidi
ya kukiendesha kikundi kwa (1)kufanya maamuzi, na (2) vitendo. Matokeo ya mafunzo
hayo sio tu kuwa wanafunzi wanajua zaidi na wenye ujuzi lakini kutayarisha washiriki
ambao wameandaliwa na kuhamashishwa kufanya vitendo.
Mafunzo
ya jamii ya usimamizi imetumia hayo kwa kukuza na kuwezesha jamii.Tazama Mafunzo
ya Usimamizi Kwa
ufafanuzi zaidi juu ya vipengele mafunzo vya uhamashishaji na usimamizi
––»«––
Haki
ya Kunakili: Phil Bartle
Imeundwa Upya: 2008.10.13
|