THIS PAGE HAS BEEN MOVED
If you are not redirected to its new location in a few seconds, please click here
DON'T FORGET TO UPDATE YOUR BOOKMARKS!
UTARATIBU WA MBINU ZA JINSIA
Mtafsiri Caroline Ndururi
Vidokezo
vya Mhamasishi
Utaratibu
wa mhamasishi wa kuinua ufahamu na usitawishaji wa usawa wa kijinsia
Muhtasari:
Huu
ni utangulizi wa baadhi ya masuala kuu ya kijinsia, na baadhi ya mbinu zinazoweza
kutumiwa na mhamasishi wa jamii.
Utangulizi:
Maandiko
haya, kama yanayopatikana kwenye tovuti hii, yameelekezwa kwa mhamasishi wa jamii,
na siyo maandishi ama makala ya taaluma.
Lengo
lake ni kujulisha mhamasishi kuhusu masuala yanayohusiana na jinsia, na kumsaidia
kukuza maarifa ili kuleta ufahamu kuhusu masuala ya kijinsia na kuelimisha jamii
na mashirika yao kuhusu uongezeko wa usawa wa kijinsia na haki.
Mheshimiwa,
Mary Nagu, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Maswala ya Wanawake na Watoto,Tanzania,alisema,
''Hatuwezi kupata maendeleo ya jamii iliyo halisi bila usawa wa kijinsia, ushiriki
wa jamii ndio elementi ya muhimu kabisa kwa kutekeleza usawa wa jinsia.'' (Personal
Communication, Istanbul, 1996)
Kwa
kweli, kazi ya jamii ni chombo muhimu cha kuleta uinuo wa ufahamu kuhusu maswala
ya kijinsia, na cha kusawazisha baadhi ya tafauti.
Jinsia
Dhidi ya Aina:
Baadhi
ya wasimamizi sugu wa kuhimili dhuluma dhidi ya wanawake wanasema neno ''jinsia''
si neno halali,iliundwa tu kutaabisha vikao vya kiasili. Bali na haya, ni muhimu
kwa mhamasishi kujielimisha kuhusu neno ''jinsia'', kwa sababu gani inatumiwa, na
umuhimu wake kwa ujenzi wa uwezo,uzalishaji wa mapato na kuwawezesha jamii wenye
mapato ya chini.
Kwanza
kabisa ni kutofautisha kati ya maneno ''aina'' na ''jinsia.''
Kwa
ufupi, ''aina'' ni kiubiologia na ''jinsia'' ni kiushirika. Sifa za kiubiolojia zinaenezwa
na kudumishwa katika vizazi kupitia majeni (na uzazi wa kingono) ilhali sifa za kiushirika
zinafunzwa, kuenezwa na kudumishwa (na viashirio wala sio majeni) kupitia mawasiliano
na utaalamu (uzazi wa kiushirika).
Tafauti
kubwa katika aina ni kati ya ''mwanamume'' na ''mwanamke'' ilhali kwenye jinsia ni
kati ya ''ume'' na ''uke''. (Utafiti wa kiubiolojia unadhihirisha ya kwamba tunaweza
kumiliki zaidi ya aina mbili, pengine kadiri ya miungano tano tofauti za kromosomu
X na Y na jeni zao.
''Ume''
au ''uke'' unatafauti sana, na hutofautiana kutoka utamaduni kwa utamaduni, na enzi
kwa enzi katika historia. Sentensi hii inadokeza ya kuwa sifa za ushirika (ume au
uke) ambazo wanadamu hutumia kwa watu tofauti, kama kiitikio kwa sifa zao za kiubiolojia,
ni holela kiutamaduni, na zinaweza kubadilishwa katika mfumo wa maendeleo ama mageuzo
mengine ya ushirika.
(Sifa
zetu za kiubiolojia zinatambulishwa kwa wingi na urithi wetu wa ujeni, na zinaweza
kubadilishwa, kwa ugumu, kupitia upasuaji, madawa, ama kupitia njia zingine za kibinadamu).
Masuala
ya Haki za Binadamu:
Ijapokuwa
maadili yanatofautiana kutoka jamii kwa jamii, nchi kwa nchi na mara kwa mara, tunaweza
kukiri ya kuwa kuna maafikiano, kwa jumla, kuhusu wema na uovu.
Ubaguzi
wa rangi ni dhana yenye upana na kwa jumla inachukuliwa kuwa ovu, ijakapokuwa kuna
uwezo wa kutambua watu wenye maadili ya ubaguzi.Itikadi yenye maana kwenye ubaguzi
wa rangi ni kwamba kuna watu wanaotambuliwa na baadhi ya sifa za kimwili (rangi ya
ngozi, nywele muundo wa mfupa) na mbaguzi anaamini ya kwamba hizo sifa za kimwili
hufunga watu kwa tabaka, na kwamba baadhi ya sifa zisizo za kimwili zitatumika wazi
kwa wote walio katika tabaka hiyo. Baadhi ya itikadi za ubaguzi za wazi ni (1) ''Wanegro
wote ni wenye asili ya kimuziki'', (2) ''Wazungu wote ni wabaguzi wa rangi'', (3)
''Wayahudi wote ni wajanja na pesa'', ama (4) ''Watu fulani ni makauleni, malaya,
mabahili, ama wenye njaa ya mamlaka,'' - na kadha wa kadha.
Itikadi
hizi za ubaguzi hutajwa mara nyingi kuhalisisha dhuluma kwa baadhi ya watu kwa njia
ya ubaguzi, ama kuhalisisha sheria zinazotungwa kuzuia ushiriki wao kamili katika
maisha ya kiraia. Inapochunguzwa, inakua wazi kuwa ubaguzi wa kijinsia ni sawa kama
ubaguzi wa rangi. Ni ubaguzi wa sifa zisizo za nje za ushiriki, na mienendo kwenye,
vitengo vya watu wenye baadhi ya sifa za kiubiolojia.
Tukiangalia
kwenye maafikiano kati ya mataifa kama vile Ilani ya Haki za Binadamu, tunaweza kupata
maadili ya manufaa kwetu. Baadhi yao ni wazo kwamba kila mtu ana haki ya huduma,
uweza, huduma za kisheria, ama ushiriki wa kiraia, bila ubaguzi wa rangi, itikadi
za kidini, ama babu nyingine zinazogawanya ubinadamu.
Mashinani,
kwenye watu walio na mapato ya chini na elimu hafifu, jamii ambazo tunazoawazwa,
maadili haya ni geni, na hata mara nyingi hayajulikani. Hii huweka mzigo wa jukumu
kwa mhamasishi; kufunza maadili haya, na kufanya kazi, kama makaimu wa mageuzi, kwa
kutekeleza maadili haya ya kiulimwengu, kama baadhi ya utaratibu wa uhamasishi.
Masuala
ya Kiuchumi na Kisiasa:
Binadamu
wote wanaweza kuchangia katika jamii zao kwa njia na viwango tofauti. Jamii huimarishwa
na hizo michango, kwa sababu, na si juu ya, hizo tafauti.
Kama
ni mazoea ya kikundi cha watu kutoshirikisha kama asilimia hamsini ya umma kwa shughuli
za mazao; basi uchimbaji wao wa shughuli za kiuchumi huzorota kwa kupoteza asilimia
hamsini ya mazao inayotarajiwa. Kwa sababu ya athari ya kichanganyiko,asilimia hamsini
ya mazao hayo yakiunganishwa, uchimbaji utazidi asilimia hamsini iliyoongezwa, labda
itaongezeka kwa mara tano zaidi. Kutoshirikisha nusu ya umma kwa sababu ya jinsia
inaathiri uchumi kwa asilimia hamsini zaidi. Kiuchumi, ni hekima kushirikisha wanawake
na wanaume kwa usawa katika uchumi wa jamii yoyote.
Alhasil,
kama ni mazoea ya kikundi cha watu kutoshirikisha asilimia hamsini ya umma kwenye
uamuzi ya kisiasa yanayoathiri jamii yote, basi uwezekano wa uamuzi hupungua. Dhana
inayoshikiliwa na jamii kuhusu hali ya baadaye na uwezo wake hukadirika. Thamani
hupotea. Ni hekima kushirikisha wanawake kwa usawa kwenye utaratibu wa uamuzi wa
kisiasa wa jamii yoyote.
Njia
ingine ya kuona na kuelewa hasara hiyo ni kutoshirikisha wanaume kwenye shughuli
za kiuchumi ama utaratibu wa uamuzi wa kisiasa. Kisayansi, hakuna sababu yoyote kudhania
ya kwamba chango la wanaume ni bora ama zaidi kwa njia yoyote kuliko chango la wanawake.
Watu
wasioshirikishwa barabara (kwa mfano wanawake) kwenye mfumo wa kisiasa na uchumi
hubuni rasilimali ya thamani isiyofaa kudharauliwa katika maendeleo ya jamii. Umaskini
utazidi bila hao.
Kisiasa
na kiuchumi, jamii itakua imara zaidi, ya anuai zaidi, ya bunifu zaidi, ya mazao
zaidi, ya usawa zaidi, wanaume na wanawake wakipewa nafasi sawa kushiriki katika
maisha yake ya kiuchumi na kisiasa.
Masuala
ya Kiutamaduni:
Kwenye
warsha ya kijamii iliyosahalishwa na wanawake wawili wachanga kutoka Wizara ya Jinsia
ya Uganda (kwa niaba ya mradi wetu wa kuwezesha jamii), Nilimskia mzee mmoja akilalama,
''Mnajaribu kuua utamaduni wetu?'' Alikua na uhakika ya kwamba ni kimila na kiutamaduni
wanawake kuchukulia wanaume wote kuwa wakuu kwao, kwamba wanawake hawafai kushiriki
kwenye utaratibu wa uamuzi wa kijamii, na kwamba jukumu la wanawake ni kuhudumia
wanaume. ''Hapana,'' mwanamke mchanga alijibu mbele ya mkutano,''Hatuathiri
utamaduni wetu,
''Tunataka kuimarisha sehemu zake bora na kutupilia mbali sehemu zisizo na manufaa.''
Wewe,
kama mhamasishi unahitaji jibu kwa wale wanabishania kuhifadhiwa kwa utamaduni wao,
wale wanahofu ya kuwa ukigeuza desturi na vikao chache basi utaangamiza utamaduni
huo.
Anza
na ufahamu wa maana ya utamaduni. (Rejea asili ya utamaduni katika makala, Utamaduni).
Utamaduni una uhai (kidubini), ushirika kuliko kiubiolojia. Una mambo yote (vikao,
miendo, itikadi) yanayofunzwa kuliko kurithiwa kiujeni. Lazima ikue na ibadili ili
ibaki hai. Kukua na kubadili inamaanisha mageuzi.
Chochote
ambacho kimehifadhiwa hakina uhai. Dagaa lazima wafe ili wahifadhiwe kwa kebe...
Achali ndani ya chupa ya kuhifadhi hayana uhai. Vifaa ndani ya jumba la makumbusho
havina uhai. Hivi vitu vyote havina mageuzi, ndio kwa maana vinahifadhiwa.
Sisi
kama wahamasishi tunaheshimu na kuadhimisha mila na utamaduni wenyu/wetu. Tunauona
utamaduni wetu ukiwa na uhai, lakini, si ule hauna uhai (hauna mageuzi) kama lugha
ya Kirumi. Lakini, kwa utamaduni wetu wa heshima uhifadhiwe, lazima ukue na ubadili;
Kwa hivyo, lazima ugeuke ili ufikiane na mazingira ya kisasa ya dunia.
Mageuzi
hayawezi kuepukika. Ijapo lazima kuwe na mageuzi, basi ni vizuri kuwe na athari kuhusu
mwelekeo wa mageuzi hayo badala ya kuyatambulisha kiutamaduni bila ya ushiriki wetu.
Ijapo lazima sheria zetu zibadili, basi ni vizuri zibadili kuelekea kwenye ilani
ya ulimwengu kuhusu haki za binadamu badala ya sheria ya kimwitu.
Kwa
muda mfupi, kusawazisha ushiriki wa kijinsia unaweza kuonekana kuwa kinyume na utamaduni,
sanasana ambako wanawake walikuwa wamedhulumiwa. Kwa muda mrefu, kwa kinyume, ushiriki
wa sawa wa wanaume na wanawake utachangia katika jamii imara, na kwa hivyo katika
uthabiti,maendeleo, na uhifadhi wa utamaduni wetu.
Ilhali
sehemu nne zilizotangulia zilifafanua asili ya jinsia kwa ushirika na kiutamaduni
na hoja ya kuboresha usawa wa kijinsia ili kuimarisha jamii, sehemu zifwatazo zinakuagiza
jinsi ya kuunda mikakati zako mwenyewe, kama mhamasishi, kwa kuzisaidia na kuongoza
jamii katika kutimiza usawa wa kijinsia zaidi na ustahiki.
Mwinuko
wa Ufahamu:
Kusuluhisha
tatizo, lazima tufahamu kama lipo.
Kumbuka
ya kwamba washiriki wa jamii lazima wasuluhishe matatizo yao ya kiushirika na kiujamii.
Kama katika maendeleo ya jamii yote, hauendelezi jamii, jamii inajiendeleza. Maingilio
yako, pamoja na mwongozo, usisimuo, elimu na usukumizi, unaweza kuleta mwelekeo,
lakini mabadiliko yanafaa kutekelezwa na washiriki.
Washiriki
wengi hawawezi kuona kuna tatizo la kusuluhishwa, ama hawataki kuliona. Washiriki
wengi hufaidika katika mamlaka hasiyo na usawa na wanaogopa mabadiliko yoyote yanayoweza
kupunguza mamlaka yao, ufahari, makadara ama mafao yao ya kiuchumi. Wale, walio na
masilahi ya kiubinafsi kama hayo, watanena ya kwamba hakuna tatizo lolote, ama wagombane
kuwa kubadilisha mila na itikadi za kiasili utaathiri utamaduni.
Jawabu
lako kwa tatizo la kwanza ni utetezi, mwinuko wa ufahamu na kuelimisha washiriki
wote wa jamii. Kwa la pili, kukabiliana na masilahi ya kiubinafsi itazingatiwa kwenye
sehemu ifwatayo.
Utaratibu
wa mwinuko wa ufahamu miongoni mwa kikundi kilicholengwa unatatuliwa kwa ubora na
mbinu za shirikishi.
Kumbuka
ya kwamba tunaelimika kwa uchache kwa kusikiza, kwa kiasi kwa kutazama utendaji,
na zaidi kwa kuhusika - kwa kutenda. Kumbuka washiriki wa jamii watachukua jukumu
zaidi kwa mradi wakikata hukumu la kuitekeleza, na wasipochukulia imetozwa kwao kutoka
nje. Lazima ''wamiliki'' mradi huo. Hizi ni kanuni za msingi za maendelezo ya jamii
kama zilivyofafanuliwa kwenye
Mwongozo
wa Wahamasishi.
Mbinu
yako kuu, basi, ni kwenye vikao vya vikundi, kuuliza maswali, kama Socrates. Usihubiri,
ubishane, ama kuhutubia washiriki. Waulize maswali yatakaowaongoza kuangalia uhali,
jamii yao, kwa mipaka ya usawa wa kijinsia.
Lakini,
haitaumiza kujumuika kibinafsi na watu wenye nabihi, rehema na wakidini na viongozi
wengine wa maono na jamii, na kuwahimiza kuhubiri, kuhutubia ama kubishana kuhusu
mada hiyo.
Maswali
kuhusu usawa wa kijinsia hayafai kuachiwa warsha maalum zinazohusika na jinsia pekee
(zinazokinga suala hilo, na mara nyingi huwa kama kuhutubia waongofu), bali yanafaa
kuhusishwa barabara katika elimu ya uongozi na uhamasishi wa jamii kutekeleza miradi
yao wenyewe.
Usitawishaji
wa Usawa wa Jinsia:
Kuna
tafauti za usawa kuu zenye haziwezi dhibitiwa kwa dunia halisi, ambamo wanaume wanapatikana
kwa wingi katika hali fulani na wanawake kwa hali nyingine, kwa ujumla zinazowadhulumu
wanawake kinyume na wanaume. Lengo la usawa wa jinsia litakua lenye kurekebisha tafauti
hizo kuu.
Kiwango
madhubuti cha asilimia hamsini kamili cha kila hali kitakua yabisi, na kigumu kufanya
kazi nacho.
Baada
ya kuona ya kwamba tokeo la usawa wa kijinsia linaambatana na thamini zetu za haki
za binadamu, na linafaidi utamaduni wetu, kisiasa na kiuchumi, basi lazima tuulizie
mbinu tunazoweza kumiliki kulitekeleza. Huu si wakati wa kumiliki mbinu ya, kujaribu
kutumia, kwote, njia wastani ya sahihisho. Kuna umuhimu wa kuchanganua kila tatizo
na kutafuta utambuzi wa kienjeji ufaalo kila tatizo. Catalina Trujillo, mradi wa
UNCHS wa Wanawake kwenye Makazi, alitumia mandhari inayojulikana sana katika muktadha
wa lengo hili: ''Tafakari kiulimwengu - Tenda kienyeji'' Tazama
UNCHS
Mageuzi
ya ushirika ikidhamiriwa, unaweza kupata watu wanaounga mkono mageuzi hayo na wanaoyapinga.
Tatizo hili kuhusu uongezeko wa ushiriki wa jamii, kwa mfano, linapatikana kwenye
mwongozo wa wahamasishi.
Watu
wanaopinga mageuzi huwa ni wale walio na masilahi ya kiubinafsi. La ajabu ni kuwa
wale walio na uzuizi watayapinga mageuzi hayo, na ni kwa sababu wanaamini watapata
hasara, hata kama hautafahamu thamani ya hasara hiyo. Watu waliodhulumiwa mara kwa
mara hukatalia kwenye minyororo hiyo kwa sababu wanadhani watapoteza ulinzi na fursa
ya kuchukua jukumu na kufanya maamuzi.
Watu
wanaoona ya kwamba watafaidika kutokana na mageuzi hayo ni wandani, ama wanaweza
kuwa wandani wako na wa watu wengine wanaotaka kutekeleza mageuzi hayo.
Mbinu
zako, kwa hivyo, nizakudhihirisha ya kwamba mageuzi yaliyopendekezwa niyakunufaisha
watu wote, mpaka wale wanaodhani watapata hasara. Mageuzi yanafaa kuonekana yenye
manufaa kwa wale wanaoweza kuyapinga ili waweze kuondoa upinzani wao, na hata waunge
mkono mageuzi hayo kwa uhodari. Kwa dhana ni rahisi, lakini ina ugumu wake.
Kifano
kingine ni kwenye kuratibu shirikisho la wafanya biashara. Kwa kuratibu shirikisho,
wanachama wote watafaidika kwa kupata ujira na kanuni za kikazi bora, wakijiunga
na shirikisho hilo.
Jambo
moja unalojua, amabalo lilifafanuliwa hapo awali, ni kwamba jamii itafaidika kwa
ushiriki wa wanaume na wanawake. Kuondoa vizuizi kwa ushiriki wa aina yoyote ya watu
itamaanisha kuwa mazao (kisiasa, kiutamaduni,kiuistlahi, kiuchumi) yatakua na tafauti
zaidi, msingi zaidi, na ubuni zaidi. Kwa jumla kutakua na uhamasishi (uwezo utaongezeka),
na washiriki wote watafaidika. Hakutakua na matatizo yoyote kuwasiliana na watu walio
na ufahamu zaidi wa ushirika na siasa. Kwa hivyo uhamasishi wako, ilivyotajwa hapo
mbeleni, haupaswi kuhusika na tafauti pekee, bali hata ufafanue faida za uongezeko
wa usawa wa kijinsia kwa ujumla na kwa kila mshiriki.
Kanuni
ya msingi ni kwamba sera inayozingatia wote itakua na manufaa kwa jamii na washiriki
wake.
Ufululizo
wa Jinsia:
Mbinu
inayotumiwa mara kwa mara katika mageuzi ya ushirika ama kwenye miradi ya maendeleo,
ni kuanzisha mageuzi hayo katika sehemu ama sekta moja, kisha, juu ya ufanifu na
mafunzo inayopatikana, kuyafululiza katika jamii yote.
Kwa
kazi yako,uhamasishi wa jamii, upungufu wa umaskini, usahalishaji wa maendeleo ya
uwezo ya mashirika, mafunzo ya wasimamizi, usitawishaji wa kujitegemea, mbinu hiyo
ya ufululizo haifai. Mfululizo wa ufahamu wa kijinsia na usitawishaji wa usawa wa
jinsia zinafaa kuhusishwa mwanzoni mwa kazi yako na kutekelezwa mpaka mwisho.
Tatizo
la kushugulikia jinsia mwanzoni katika sehemu kadhaa,ilivyofafanuliwa, husababisha
ukingaji wa masuala. Ukiandaa warsha ya kijinsia, utawavutia zaidi washiriki wanaofahamu
tatizo hilo na wanaounga utatuzi. Ukishirikisha ufahamu wa jinsia na kutunga mbinu
za usawa wa kijinsia kama mada mahsusi kwenye vikao vyako vyote vya mazoezi, utafaulu
kuwashirikisha watu wanaofaa na ujumbe huo.
Warsha
inayozingatia jinsia pekee itakua na umuhimu unaporatibu Mafunzo ya Wafundishaji
ama unapokua na mkutano na wafanyikazi wako ama watu wakujitolea; basi unafaa kujihusisha
na ustawishaji wa mbinu badala ya mwinuko wa ufahamu. Hautakua ukitekeleza mbinu
ya kijinsia, bali utakua ukitayarisha wafanyakazi wako na wanaokuunga katika kupanga
mbinu ya kijinsia.
Kwa
harakati zako zote,uhamasishi wa jamii, utungaji wa vikundi, mafunzo ya wasimamizi,
maendeleo ya uwezo, upunguo wa umaskini, unahitaji kuhusisha mwinuko na usawa wa
kijinsia. Ufululizo unafaa kushirikishwa mwanzoni.
Kimalizio:
Mwinuko
wa ufahamu wa kijinsia na usitawishaji wa usawa wa kijinsia ni sehemu muhimu wa uhamasishi,
mafunzo ya wasimamizi, maendeleo ya uwezo na upunguo wa umaskini.
Unahitaji
kuunda mbinu mahsusi,tambua wale wanaoweza kupinga mageuzi hayo, wafafanulie manufaa
kwao, na uhusishe haya yote mwanzoni mwa kazi yako.
Hakuna
utaratibu mahsusi ama seti ya harakati za kufuata.
Unahitaji
kuchunguza tatizo, utumie kanuni zinazopatikana katika makala haya, na utengeneze
mbinu ya kienyeji itakayokua na fanaka.
––»«––
Warsha
Hakimiliki:
Phil Bartle
Ilisasishwa: 2009.02.13
|